Brighton anaota ndoto ya ajabu
akiwaona watu waliokufa siku nyingi kwa kujiua wakiwemo mzee Mboma, Patrick,
James na Anna. Baada ya ndoto hiyo anazongwa na mwanadada Sharifa
anayemsababishia kesi ya mauaji ya mpangaji wake, yaani Kishoka. Kesi
inaunguruma mahakamani kisha anajikuta akihukumiwa adhabu ya kunyongwa mpaka
afe kwa kosa la mauaji ya Kishoka, kosa ambalo alikuwa hajalitenda. Akiwa
gerezani akisubiri tarehe za kunyongwa anakutana na Mack, jamaa aliyekuwa
amenunua nyumba iliyokuwa ya marehemu James, naye Mack anaanza kumhadithia kisa
kilichompelekea afungwe jela.
Kwa
kusimuliwa na Mack, Brighton anayasikia mengi kuhusu mali alizokuwa amerithi kutoka
kwa marehemu kaka yake kwa kila aliyekuwa amemuuzia aliishia kupatwa na
matatizo akiwemo Mack mwenyewe. Hatimaye siku ya kunyongwa inafika kweli, hata
hivyo anajikuta anakolewa kimiujiza na msichana aliyemsingizia kuua, yaani
Sharifa, anatolewa gerezani na kuwa huru kabisa. Sasa endelea...................
‘Ina
maana Mapara keshakuwa mbunge siku hizi, au ndiyo ile tabia ya kujiweka ‘matawi
ya juu’ na kulazimisha uheshimiwa pale mtu anapozinyaka.’ Nilizidi kuwaza huku
nikitafuta majibu ya kumpatia jamaa huyo aliyekuwa kavimbisha tumbo lake kwenye
kimlango kidogo cha geti langu.
Kwa
kweli ilikuwa ikiniwia ugumu jinsi ya kuanza kuuliza kuhusu huyo mhesimiwa
aliyekuwa anasemwa yuko nje ya nchi. Wazo la kwamba Mapara keshakuwa mtu mkubwa
kiasi kwamba mpaka akafikia hatua ya kuitwa mheshimiwa; lilikuwa haliniijii
kabisa akilini.
Mapara
alikuwa hajasoma sana kiasi cha kuweza kugombea hata udiwani. Alikuwa kaishia
darasa la saba tu, tena la saba lenyewe alikuwa ni ‘bongo lala’ kitu ambacho
asingeweza kugombea kutokana na mabadiliko ya utandawazi tuliyonayo siku hizi.
Siku
hizi udiwani ni kuanzia ‘form four’, tofauti na siku za nyuma ambapo utamkuta
diwani darasa la saba. Mambo yamebadilika, watu wameshaupumuzisha uongozi wa
kianalogia na sasa hivi ni mwendo digitali mpaka kwenye umwenyekiti wa
kitongoji ama umwenyekiti w serikali za mtaa.
Sababu
hiyo ndiyo ilizidi kuweta fukuto ndani ya kichwa changu. Nikawa nashindwa
nianze vipi kuuliza habari za huyo Mapara niliyekuwa nimemuachia nyumba yangu
pamoja na miradi yangu yote.
“Kwani
hapa ni kwa nani?” Nilijikuta naropoka kuuliza.
Jamaa aliguna kwanza kisha akasema,
“Watu wengine sijui mkoje, kwa hiyo wewe
wakati unatoka huko ulikuwa unajua hapa ni kwa nani?” Swali hilo lilielekezwa
kangu.
Akili
yangu ilizidi kukorogeka na kuvurugika. Nikajikuta nimeropoka tena,
“Kwani Mapara ndiyo mwenye nyumba hii?”
“Siyo bure wewe ni zuzu, maana tangu umefika
sijaelewa hata kimoja unachoniambia. Hebu nenda moja kwa moja kwenye pointi
yako ya msingi iliyokuleta hapa.” Alimaka jamaa huyo.
Nikaona
alichokuwa amekiongea ni kitu cha msingi, nikaona niende moja kwa moja kwenye
pointi. Hata hivyo nilikuwa naogopa kumwambia kuwa nimeponea chupuchupu
kunyongwa nikihofia siri itafichuka.
“Sikiliza
kaka, mimi ni mwenyeji kabisa wa mji huu ila nilitoka miaka kadhaa iliyopita.
Sasa wakati natoka aliyekuwa akiishi hapa ni jamaa mmoja Mapara, la sijui mpaka
sasa anakaa hapa?”
“Alaaha! Sasa nimekusoma. Hapa haishi huyo
Mapara unayemsema, hapa ni kwa mheshimiwa mbunge na ni mwaka wa tatu sasa
anaishi hapa, huyo uliyemtaja mimi hata simjui.”
Kauli hiyo ilinifanya niishiwe nguvu. Nilizidi
kuchoka. Mtu pekee ambaye nilikuwa nikitegemea aje awe msaada mkubwa kangu
alikuwa ni Mapara, naye nilikuwa nimemkosa. Mtihani uliofuata ni wa kujiuliza
pa kumpata.
Wakati
wa sakata la kifo cha Kishoka, Mapara alikuwa ndiyo mtu pekee aliyekuwa anakuja
kunisalimia kituo cha polisi pamoja na kuniletea chakula. Hata nilipohamishwa
na kupelekwa mahabusu ya magereza aliendelea kuwa anakuja kuniona.
Ndipo nilipomkabidhi
funguo za nyumba yangu pamoja na majukumu mengine ya kusimamia miradi yangu.
Hakuwa
rafiki yangu ki vile japokuwa tulikuwa tunafahamiana sana kwa vile yeye ndiye
alikuwa mmoja wa watu walionipokea kwenye mtaa huo wakati nahamia.
Baada
ya kuambiwa hivyo nikawa njia panda. Nikaanza kujiuliza sijui niende alipokuwa
akiishi kwa kipindi kile ambapo alikuwa amepanga chumba kwenye nyumba moja
iliyokuwa na wapangaji lukuki!
JE, NINI KITAFATIA? USIKOSE....
UTAJIRI AU MALI ZA NDAGU NA MAJINI NDANI YA MASAA 48 MPAKA 72. KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA MAFANIKIO.
ReplyDeleteEveryone
Leo Natoa somo bure kuhusu Mali za ndagu,
Unaweza kujiuliza mali za NDAGU ni nini?
Dokta Mdiro call/whatsup +255 742162843.
Ndagu ni dawa ambazo hutengenezwa kwa mkusanyiko wa taratibu fulani ambazo hufanyika kwa pamoja ikilenga jambo fulani.
Hasa malengo makuu ya ndagu ni
1.kutengeneza mali
2.kulinda Mali.
Ndagu hizi hutumia nguvu ya wazee(Mizimu)
Sasa yapo nikupe maana ya mizimu ni nini?
MIZIMU NI NINI?
Mizimu ni roho za wazee wetu (wa ukoo) toka katika pande zote mbili Baba na Mama ambao ni babu na bibi toka kwa baba na babu na bibi toka kwa Mama,roho hizi huja na kuwa na sisi pale tunapozihitaji au zinapotuhitaji....!
kwanini Mizimu huja kwetu au kwaini tunaiita?
-UDUGU, kumbuka roho hizi ni zile za waze wetu (ancestors) ambao walizaa baba na mama zetu hivyoo kuja au kuwaita hutokana na Udugu
ULINZI, roho zote zisizo na mwili huona yasiyoonekana kama Uchawi na magonjwa hivyoo Wazee wetu huja na tunawaita watuambie haya tusiyoyaona.
MILA, utamaduni na desturi zetu hututaka tufanye mambo yaliyo katika mpangilio ulio sahihi kama kuwapa wazee heshima na kusikiliza yale wanayotuambia.
Wazee hawa hutupatia mali kama zawadi lakini kwa masharti fulani maalumu hii ni tofauti na majini.
Aina za ndagu zipo sita kunazile ambazo unaweza kufanya sehemu ulipo na zile ambazo unaweza kufanya kwa kunifuata yaani tukiwa pamoja hii ni kutokana na sababu mbalimbali kama wengine kutokuwa na ghalama za safari hivyo unaweza kufanya sehemu ulipo na jambo lako kukamilika.
Ndagu ambazo ni lazima tuwe pamoja ni 4.
1.Kutoa kitu.
2.Mimba.
3.Utasa.
4.Ndugu 3.
Ndagu ambazo unaweza kufanya sehemu ulipo ni 2.
1. Ulemavu.
2.Wanyama.
Angalizo!!! Kwa msaada piga simu husijaribu jambo bila maelekezo ya dhati.
Karibu sana na uwe na nia ya dhati.
DOKTA MDIRO Namba call/whatsup +255 742162843