Friday, November 29, 2013

MIRATHI YA KAKA sehemu ya 49

Brighton anaota ndoto ya ajabu akiwaona watu waliokufa siku nyingi kwa kujiua wakiwemo mzee Mboma, Patrick, James na Anna. Baada ya ndoto hiyo anazongwa na mwanadada Sharifa anayemsababishia kesi ya mauaji ya mpangaji wake, yaani Kishoka. Kesi inaunguruma mahakamani kisha anajikuta akihukumiwa adhabu ya kunyongwa mpaka afe kwa kosa la mauaji ya Kishoka, kosa ambalo alikuwa hajalitenda. Akiwa gerezani akisubiri tarehe za kunyongwa anakutana na Mack, jamaa aliyekuwa amenunua nyumba iliyokuwa ya marehemu James, naye Mack anaanza kumhadithia kisa kilichompelekea afungwe jela.
Kwa kusimuliwa na Mack, Brighton anayasikia mengi kuhusu mali alizokuwa amerithi kutoka kwa marehemu kaka yake kwa kila aliyekuwa amemuuzia aliishia kupatwa na matatizo akiwemo Mack mwenyewe. Hatimaye siku ya kunyongwa inafika kweli, hata hivyo anajikuta anakolewa kimiujiza na msichana aliyemsingizia kuua, yaani Sharifa, anatolewa gerezani na kuwa huru kabisa.
Anaporudi kwake anakuta nyumba yake ishauzwa na mtu aliyekuwa amemwachia.  Sasa endelea...................

Wakati nagonga wimbo uliokuwa unakita ulifikia mwisho, hapo hapo na mimi nikagandamizia kuendelea kugonga ili nipate kusikika. Kabla wimbo mwingine haujaanza kusikika niliweza kuona mlango ukifungulia. Ndipo alipotoka kijana ambaye nilikuwa namfahamu; alikuwa akiitwa Benja.
            Hata hivyo hakuonyesha dalili zozote za kuweza kunitambua. Nilikuwa nimebadilika si mchezo. Sikuwa kama Brighton wa kipindi kile, enzi hizo kina Mapara na hao kina Benja walikuwa wanapenda kuniita pedeshee mtoto, jina ambalo nilikuwa nalipinga vikali kwani nilikuwa sipendi majisifu.
            Nilipogundua kwamba hajanifahamu nilianza kujiuliza,
‘Sijui nimkumbushe, sijui nijikaushe tu ili siri yangu izidi kudumu. Lakini nikijikausha atanipa michapo yote kuhusu Mapara?” Nilizidi kuwaza na kuwazua wakati tukisalimiana.
            Suala la kujikausha ndilo lililopitishwa na halmashauri ya ubongo wangu japokuwa kama angekuwa mgumu kunieleza habari nilizokuwa nazihitaji basi ningejifunua kwake.
            Baada ya salamu mazungumzo yaliendelea,
“Karibu bwana!”
“Asante!”
“Karibu pita ndani.”
“Asante lakini nipo haste haste kidogo, namulizia Mapara.”
“Unamuulizia Mapara?”
“Ndiyo!”
“Ni nani yako huyo Mapara?”
“Ni rafiki yangu!”
“Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni lini?”
“Ni miaka mingi kidogo lakini sikumbuki”
            Maswali ya Benja aliyokuwa akiuliza mfululizo utadhani naye ni polisi yalianza kunikera. Hata hivyo niliona nikianza kumjibu utumbo sitafanikisha nilichokuwa nakihitaji. Nililazimika kuwa mpole kama simba jike anapozaa ili nifanikishe suala langu, suala la kupata habari za Mapara.
            Niliendelea kjitahidi kumjibu kila swali alilouliza.
“Wewe ni mwenyeji wa wapi?”
“Ni mwenyeji wa mji huu huu ila nilisafiri siku nyingi.”
“Dah! Huyu Mapara ana miaka mingi sana hayupo nchi hii!”
“Yupo nchi gani sasa?”
“Hata mimi sijui ila ninachojua ni kwamba huwezi ukampata mji huu wala nchi hii.”
            Mpaka hapo nilikuwa nimeishiwa maji. Mambo yalizidi kuniwia ugumu baada ya kuambiwa kuwa Mapara alikuwa yupo nchi za ng’ambo.
            Hata hivyo nilijua dhahiri ya kwamba Benja alikuwa ananificha kunieleza habari kamili. Niliamini kabisa kuwa alikuwa anajua mambo mengi sana kuhusu Mapara kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu sana.
            Baada ya kuona mambo yamenikaa vibaya sikuwa na budi kunyolewa. Nilimuomba Benja tuingie ndani kwake ili nikamuelezee matatizo yangu kwani nilikuwa na matatizo makubwa.
            Benja hakukataa. Alinikaribisha ndani nami nikaingia. Tulipofika ndani nilimweleza kinaga ubaga bila kumficha kitu chochote kuhusu kesi yangu ilivyoenda, hukumu mpaka kutoroka kwangu siku hiyo ambayo ilikuwa ndiyo siku ya kunyongwa.
            Alistaajabu sana kusikia hivyo.
“Unajua nilikuwa nakufananisha kwa mbaali lakini nikawa najiambia mwenyewe itawezekanaje mtu aliyehukumiwa kunyongwa aonekane tena uraiani? Na ingekuwa kwa msamaha wa rais basi tungesikia kwenye vyombo vya habari.”
            Kabla hatujaanza hata maongezi yetu Benja aliniambia nimsubiri kidogo, alitoka nje na kwenda sehemu ambapo sikukujua. Huku nikiwa ndani niliendelea kusikiliza nyimbo za mziki wa kizazi kipya ambao niliuacha ndiyo kwanza unachipuka.
            Hata hivyo nilihisi mabadiliko makubwa sana kwenye mziki huo kwani nyimbo zilikuwa na ubora wa hali ya juu kushinda enzi zile bado sijafungwa. Kweli kuwa jela ni sawa na kutokuwa kwenye hii dunia kwani unakuwa hujui kinachoendelea uraiani.
            Baada ya muda usiozidi nusu saa niliona mlango ukifunguliwa, ndipo alipotokea Benja akiwa na kifuko kaning’iniza ambamo kulikuwa na chakula.
            Alinitengea nami nikaanza kula. Kusema kweli nilikuwa na njaa ya kufa mtu. Tumbo nilikuwa likisokota kwa njaa si mchezo. Nilianza kula chakula kilichokuwa kimeletwa na Benja kutoka mkahawani.
            Nilipomaliza kula mazungumzo yalianza. Shauku yangu kubwa ilikuwa ni kusikia habari za Mapara. Hata hivyo kwa wakati huo nilikuwa na uhakika wa kusikia habari zote za Mapara kutoka kwa Benja kwani ukaribu wao ulikuwa ni kama pete na chanda.

JE, BRIGHTON ATAAMBIWA HABARI GANI ZA MAPARA NA MWENYEJI WAKE BENJA? JIBU LIPO TOLEO LIJALO.

1 comment:

  1. UTAJIRI AU MALI ZA NDAGU NA MAJINI NDANI YA MASAA 48 MPAKA 72. KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA MAFANIKIO.
    Everyone
    Leo Natoa somo bure kuhusu Mali za ndagu,
    Unaweza kujiuliza mali za NDAGU ni nini?

    Dokta Mdiro call/whatsup +255 742162843.

    Ndagu ni dawa ambazo hutengenezwa kwa mkusanyiko wa taratibu fulani ambazo hufanyika kwa pamoja ikilenga jambo fulani.

    Hasa malengo makuu ya ndagu ni
    1.kutengeneza mali
    2.kulinda Mali.

    Ndagu hizi hutumia nguvu ya wazee(Mizimu)
    Sasa yapo nikupe maana ya mizimu ni nini?

    MIZIMU NI NINI?

    Mizimu ni roho za wazee wetu (wa ukoo) toka katika pande zote mbili Baba na Mama ambao ni babu na bibi toka kwa baba na babu na bibi toka kwa Mama,roho hizi huja na kuwa na sisi pale tunapozihitaji au zinapotuhitaji....!
    kwanini Mizimu huja kwetu au kwaini tunaiita?
    -UDUGU, kumbuka roho hizi ni zile za waze wetu (ancestors) ambao walizaa baba na mama zetu hivyoo kuja au kuwaita hutokana na Udugu

    ULINZI, roho zote zisizo na mwili huona yasiyoonekana kama Uchawi na magonjwa hivyoo Wazee wetu huja na tunawaita watuambie haya tusiyoyaona.

    MILA, utamaduni na desturi zetu hututaka tufanye mambo yaliyo katika mpangilio ulio sahihi kama kuwapa wazee heshima na kusikiliza yale wanayotuambia.

    Wazee hawa hutupatia mali kama zawadi lakini kwa masharti fulani maalumu hii ni tofauti na majini.

    Aina za ndagu zipo sita kunazile ambazo unaweza kufanya sehemu ulipo na zile ambazo unaweza kufanya kwa kunifuata yaani tukiwa pamoja hii ni kutokana na sababu mbalimbali kama wengine kutokuwa na ghalama za safari hivyo unaweza kufanya sehemu ulipo na jambo lako kukamilika.

    Ndagu ambazo ni lazima tuwe pamoja ni 4.
    1.Kutoa kitu.
    2.Mimba.
    3.Utasa.
    4.Ndugu 3.

    Ndagu ambazo unaweza kufanya sehemu ulipo ni 2.
    1. Ulemavu.
    2.Wanyama.

    Angalizo!!! Kwa msaada piga simu husijaribu jambo bila maelekezo ya dhati.

    Karibu sana na uwe na nia ya dhati.

    DOKTA MDIRO Namba call/whatsup +255 742162843

    ReplyDelete