Friday, September 13, 2013

HII ITAKUCHEKESHA AU UTABAKI UMEUCHUNA? IKIKUCHEKESHA ANGUSHA BONGE LA LIKE NA U-COMMENT IKIBIDI.

Siku moja Papa Mtakatifu (wamiaka ya nyuma kidogo kabla hujazaliwa) alikuwa anaenda shoping na dereva wake. Siku hiyo alijisikia kuendesha gari mwenyewe hivyo dereva akakaa kwenye sit ya pembeni.
Wakiwa njiani trafic aliwasimamisha, alipochungulia ndani ya gari alimuona Papa anaendesha gari, baada ya kuona hivyo alitoka nduki na kwenda kumwita mkuu wake.
Mkuu wake naye alipofika akachungulia ndani ya gari na kumuona Papa kajituliza kwenye kiti cha dereva, Mkuu huyo akatoka nduki.
Trafic mdogo alipoona mkuu wake anakimbia na yeye aliunga tera bila kujua kilichokuwa kinamfanya mkuu wake huyo akimbie.
Wakati wanakmbia huku wakiwa wameongozana, Trafic mdogo alimuuliza mkuu wake,
"Mkuu vipi tena unakimbia?"
Yule mkuu akajibu,
"KAMA PAPA AMEKUWA DEREVA, YULE ANAYEENDESHWA KAMA SIYO YESU BASI NI MUNGU MWENYEWE!!!!

No comments:

Post a Comment