Thursday, September 19, 2013

HIKI NI KIOJA CHA LEO!

Siku moja padri alitangaza kanisani kila mwanaume atoe mchango kulingana na uzuri wa mke wake,
basi watu wakaanza kutoa.
Wengine wakatoa sh. 50,000/=, wengine wakatoa sh.30,000/= na wengine sh.20,000/=.
Kuna jamaa mmoja yeye akatoa sh.500/=,
Padri akamuuliza jamaa,
"Wewe umetoa sh.500 tu ina maana mkeo siyo mzuri?"
Jamaa akajibu,
"Tena ukimuona utanirudishia na chenji!"

No comments:

Post a Comment