SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA........
Aliniacha
na kwenda zake, nikiwa bado nipo kwenye kitanda changu cha sita kwa sita, niliendelea
kuitafakari ndoto ambayo nilikuwa nimeiota muda mfupi uliopita. Maneno ya Anna
yenye ujumbe mzito yalizidi kujirudia kichwani mwangu.
SASA ENDELEA.......
Niliangalia
saa yangu ya mkononi, nikaona masaa yanayoyoma, saa kumi na nusu ilikuwa
inaelekea. Wazo la kwenda ufukweni kupunga upepo lilinijia, nikaenda kuoga
kwanza kabla ya kuanza safari yangu ya kuelekea ufukweni. Baada ya kuoga ‘nilitupia
pamba’ za kufa mtu mwilini mwangu; kaputura ya
jinzi na fulana yenye mikono ya kuishia mabegani.
Nilienda
kwenye ‘dressing table’ langu kisha nikajipulizia marashi, nikaanza kwenda
nilikokuwa nimekusudia kwenda. Nikiwa njiani nilizidi kuumiza pua za watu waliopita
karibu yangu kwani marashi niliyokuwa nimejinyunyiza yalikuwa na harufu kali.
Huku
nikitembea taratibu nilianza kuisikia harufu ya bahari, mara nikaanza
kuukanyaga ufukwe. Nikiwa naambaa ambaa kandokando mwa bahari, nilimuona mwanadada
amekaa mbele yangu. Nilianza kumfuata ili nikampe ‘hai’, na ikibidi tupigepige
soga kubadilishana mawazo.
Nilipomkaribia
akainuka, hapo ndiyo niliweza kuushuhudia uzuri aliojaaliwa na Muumba. Kichwani
nywele ndefu, kifuani maziwa yaliyojaa kiasi, kiunoni palikuwa pamekatika
kidogo kisha pakafuatiwa na wowowo la wastani.
Nilizidi
kukoshwa na hipsi zake sanjari na mguu wake wa bia. Mwanadada huyo alikuwa kavaa
kipedo pamoja na kitopu. Kwa jinsi alivyokuwa ametokelezea nilijikuta
nikivutiwa naye kabla hata sijaanza kuongea naye.
Kabla
sijafika alipokuwa nilimuona kajinyosha kisha akaanza kuchapa lapa, bila
kujishauri mtu mzima nilijikuta nikiropoka kwa nguvu,
“samahani dada, naomba kuzungumza na wewe
kidogo.”
Licha ya kutanguliza
neno la kiungwana, yaani samahani, mwanadada huyo hakusimama wala hakugeuka
kunitazama.
Nilianza
kumfuata kwa nyuma nyuma, nilipoanza kumfuata nilishangaa kumuona anaanza kukazana. Nilishindwa kuelewa ni kwa
nini alikuwa muoga kiasi hicho, nilimuita tena kwa mara ya pili lakini
aliendelea kunichunia.
“Wewe dada, inamaana
hujanisika au hujanielewa?” Hilo ndilo swali nililomtwanga huku nikimfuatia kwa
nyuma.
Kwa
mara ya kwanza niliisikia sauti yake nyororo, sauti yenye kuweza kumtoa nyoka
pangoni ama kumtoa sungura kwenye kichuguu. Sauti yake adimu ni moja ya sauti
ambazo huaminika kuvuta mvua mpaka ikanyesha hata kama ni kiangazi.
“Utanisamehe kaka
yangu kwa sababu nina haraka kwelikweli, ila usijali, nitakuja kwako kesho
asubuhi!” Alinijibu bila ya kugeuka kuniangalia.
JE, MSICHANA HUYO NI NANI? PIA ATAKUBALI
KUONGEA NA BRIGHTON? ITAENDELEA........
No comments:
Post a Comment