Ilipoishia....
‘Nitapona
kweli leo?’ Huu ni mfano wa baadhi ya maswali yaliyokuwa yanayosumbua akili
yangu kwa wakati huo. Nilikosa majibu ya maswali yangu, nikaishia kujisemea
Mungu yupo.
Sasa endelea....
Tetemeko lilikoma
ghafla, pakawa shwari tena, lakini giza lilikuwa lipo palepale. Mvua kubwa
ilianza kunyesha, mwanga na miungurumo ya radi nilizidi kuvishuhudia.
Nilibaki nimeduwaa
baada ya kugundua kuwa pale nilipokuwa silowi licha ya mvua kubwa kuendelea
kunyesha. Hakuna hata tone moja la maji lililokuwa likinifikia utadhani
nilikuwa chini ya mwamvuli, nilizidi kuchanganyikiwa.
Hata kwa chini maji
hayakunigusa hivyo nyayo zangu zilikuwa kavu. Lakini mvua nilikuwa naishuhudia
ikinyesha, tena ni bonge la mvua.
Nilibaini kuwa kumbe
nilikuwa nipo juu ya kilima baada ya mwanga wa radi kumulika. Lakini hapakuwa
hata na mwamvuli juu yangu licha ya kutoangukiwa na tone hata moja.
Mara niliona kitu
kama shuka jeupe kikishuka kutoka angani. Nilikisubiri kwa hamu kitu hicho ili
nione ni nini kitatokea.
Woga ulianza
kupungua. Siyo kwa kuwa nilikuwa nimeyazoea mazingira; la hasha! Ulipungua
kutokana na kukata tamaa nikijua kuwa kuokoka kwangu ni asilimia 0.0025. Nilijipa
uhakika wa kupoteza uhai endapo kudura za Mwenyezi Mungu zisingechukua nafasi.
Kitu hicho kilizidi
kuteremka taratibu, tena kilikuwa wima mithili ya kitambaa cha sinema. Japokuwa
giza lilikuwa limetanda angani kote, kitu hicho kiling’ara na niliweza
kuushuhudia mng’ao wake. Shauku ya kutaka kuona kitakachotokea ilizidi
kunishika, moyo wa woga haukuwepo tena kwa wakati huo.
Kitu hicho kilianguka
chini, moshi mwingi niliushuhudia kilipokuwa kimeangukia. Moshi uliendelea
kutoka mahali hapo lakini kitu hicho mfano wa shuka kilikuwa hakionekani tena.
Kufumba na kufumbua
niliwaona watu katikati ya moshi huo, nikashindwa kujua idadi yao kamili kwa
sababu walikuwa wanatembeatembea bila ya kutulia. Licha ya moshi mwingi kutanda
eneo hilo, watu hawa walionekana ‘live’ tena bila chenga.
Nilizidi
kuchanganyikiwa nilipoanza kuwatambua baadhi yao, kilichokuwa kinanishangaza ni
kwamba kila niliyemtambua alikuwa kashatangulia mbele ya haki tukamzika, yaani
namaanisha alishakufa kitambo.
Itaendelea......
No comments:
Post a Comment