ILIPOISHIA........
Kichwa changu sasa nilianza kukiona
ki chepesi, uzito kiliokuwa nao mara baada ya kugutuka kutoka ndotoni nikawa siuhisi
tena. Niliamua kuanza kurudi nyumbani kwani machweo nayo yalikuwa yamewadia.
*******************************
SASA ENDELEA.......
Ilikuwa
ni asubuhi, kwa muda huo nilikuwa nipo kwenye meza ya chakula nikipata kifungua
kinywa; supu ya kuku na mikate ya boflo.
Mara nilisikia
kengele ya getini ikinijuza kuwa kuna mgeni pale getini. Nilimuomba Kishoka aende
kumsikiliza mgeni aliyekuwa anapiga hodi kule getini kwani mimi nilikuwa
ninakula wakati yeye alikuwa hali. Naye bila ubishi aliondoka na kwenda getini.
Punde
si punde alirudi, akaja na taarifa iliyosema kwamba mgeni aliyekupo pale nje
kakataa kuingia ndani hivyo ananitaka niende tukaongee palepale nje. Nilipomuuliza
Kishoka mwonekano wa mgeni huyo upoje, alinieleza jinsi alivyokuwa. Mwonekano
wa mgeni huyo kwa mujibu wa maelezo ya Kishoka ulionekana kuendana na mwonekano
wa msichana niliyekuwa nimemuona jana yake kule ufukweni.
“Umemuuliza
jina?” Nilimuuliza tena Kishoka.
“Ndiyo nimemuuliza.”
“Akakwambia anaitwa nani?”
“Alichonijibu ni kwamba nije nikuambie kuwa
mlionana naye jana kule ufukweni na mkapeana miadi ya kuonana leo asubuhi.”
Nilifurahi sana
kusikia kuwa mrembo wa jana aliyejifanya kudengua kaingia kwenye anga zangu
mwenyewe.
Niliinuka
na kuachana na supu yangu haraka kisha nikaenda moja kwa moja mpaka getini
kumwangalia mgeni huyo. Nikiwa naelekea huko getini nilijaribu kujifutafuta
midomo yangu ili kuondoa mabaki ya boflo na mchuzi wa supu ya kuku.
Nilifika
mpaka getini, nikafungua geti na kuangalia pale nje, cha ajabu sikuona mtu
yeyote. Nikaanza kujiuliza mgeni aliyekuwepo hapo kaenda wapi? Kusema kakaa
sana mpaka akachoka kusubiria huo ni uongo kwani ulikuwa haujapita muda mrefu
sana tangu Kishoka aingie ndani kuniita, sikujua alikokuwa kaelekea.
Hata
kama angekuwa kaghairi kunisubiri akaondoka, haiwezekane nisimuone wakati njia
ya kutoka kwangu kuingia kwenye barabara ni ndefu kiasi, ni kama mita mia moja
kutoka kwenye geti la nyumba yangu mpaka kufika kwenye barabara kuu.
Nilijaribu kuangaza
kwenye njia lakini sikuona mtu. Nikaamua kurudi ndani kuendelea kushambulia
boflo zangu na supu yangu ya kuku.
DUH! KIJANA KAZI ANAYO, HUYO
MWANADADA NI NANI NA KAPOTELEA WAPI? USIKOSE SEHEMU YA 11.
No comments:
Post a Comment