Dongo janja alitumwa dukani na mama yake kwenda kununua njegere. Akiwa njiani njegere moja ilidondoka ikabiringika.
Alipoona hivyo akasema,
"Ahaa, kumbe mnajua kutembea!"
Akazimwaga zote chini huku akisema,
"mimi natangulia mtanikuta nyumbani"
Alipofika nyumbani akaulizwa na mama yake,
"njegere ziko wapi?"
Naye akajibu,
"zipo njiani zinakuja!"
Mama akabaki domo wazi!
No comments:
Post a Comment